Saturday 4 January 2014

JINSI YA KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA YA KUUZA VINYWAJI (BAR)

Na Victor Katunzi>>



Ni dhahiri kwamba wajasiriamali wengi wamekuwa wakijiuliza ni njia gani wazitumie katika kuanzisha,kukuza ama kuboresha biashara zao za kuuza vinywaji ili wapate kunufaika na faida kubwa.
Kama wewe pia ni mmojawapo kati ya wajasiriamali wanaotafuta mafanikio makubwa kwa kufanya biashara ya namna hii utakuwa umewahi kujiuliza maswali kama haya;
·        Je, mtaji wa biashara hii (bar) ni kiasi gani?
·        Mbona baa ya huyu inalingana na ile kwa mwonekano lakini yule anamafanikio zaidi kuliko huyu?
·        Nitapajaje wateja wengi kila siku?

Majibu ya maswali yako yote ya kwanini na kivipi ni rahisi tu, zifuatazo ni mbinu zinazoweza kukuwezesha kufanikiwa sana katika biashara yako ya vinywaji au 'BAR'.

1.Fanya Maandalizi ya awali {Weka nia na malengo ya biashara yako (Ni vema Ukiandika)}
Ili kufanikiwa katika biashara hii kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote,kitu cha kwanza kufanya ni kuweka nia na malengo au matarajio yako baada ya muda fulani. Kwa mfano, lengo lako la kwanza linaweza kuwa baada ya miezi sita, biashara hii iwe imekuzalishia faida kubwa inayoweza kutosha kuwa kama mtaji wa kufungua biashara nyingine n.k.

Ni lazima pia kuainisha mahitaji yote yanayohitajika kuanzisha biashara yako ikiwemo gharama ya ujenzi, malipo ya wahudumu (kwa miezi sita ya mwanzo), jinsi ya kufanya malipo, Gharama za bidhaa (vinywaji), friji, vyombo na  samani za kukalia wateja.
Umakini wa hali ya juu unahitajika katika kufanya upembuzi yakinifu wa gharama za mahitaji ya biashara na muda wa kutosha pia unahitajika ili kupata bei sahihi.

2.Jiandae kiuchumi
Baada ya kufanya maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kufahamu kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuanda biashara bila mawaa yoyote, sasa unaweza kujiandaa kiuchumi kwa kukusanya taratibu na kudunduliza pesa kwa ajili ya kufungua biashara (bar). Kama pesa ipo tayari ni vema kuihifadhi vyema na kuhakikisha haiingiliani na matumizi mengine.

3.Chunguza eneo unalohitaji kufanyia biashara
Eneo unalohitaji kuweka bar yako linanakiwa kuwa sehemu ambayo imezungukwa na wahitaji wa  aina ya vinywaji unavyotaka kuuza. Kwamfano, eneo liwe sehemu ambayo ni rahisi watu kuhitaji kuja kupumzika baada ya kazi au kukutana na marafiki na sio karibu na Makanisa wala Misikiti au eneo lolote ambapo unaweza kuwakera watu wenye misimamo tofauti ya kiimani.

4.Jenga Bar yako kwa jinsi ya kumvutia macho ya mteja (kistarehe)
Wateja wengi hupenda bar yenye mandhari mazuri ya kuvutia macho ikiwa ni pamoja na usafi wake na mpangilio wa counter, maeneo/vyumba vya kunywea na sehemu za starehe nyingine kama 'pool table' na Muziki/Tv. Vyoo pia vinatakiwa kuwa visafi muda wote ili kuvutia wateja kuendelea kuja katika bar yako kila watakapohitaji kunywa.

5.Ajiri wahudumu wenye mwonekano na lugha nzuri ya biashara
Kufanikiwa kwa Biashara kunategemea sana mahusiano kati ya wateja na watoaji wa huduma. Wahudumu wa Bar yako wanatakiwa kuwa wenye mwonekano na lugha nzuri kwa wateja, wasafi,wakarimu na wasiowahi kukasirika wakati wa kuwahudumia wateja. Wahudumu wenye sifa zilizotajwa hapo juu wanafaa na ndio hitaji la wateja wako wengi kama si wote.

6.Hakiki hesabu za mauzo ya kila siku
Unatakiwa kufanya hesabu za mauzo yanayokusanywa kila siku na kufahamu aina za vinywaji vilivyonunuliwa (kila aina kwa idadi yake). Uhakiki wa hesabu za mauzo ya kila siku yatakupa wastani wa mauzo ya kawaida kila siku, kwa wiki,mwezi na mwaka. Yanakupa pia uwezo wa kukadiria mauzo ya chini kabisa (minimum) na mauzo ya juu kabisa (maximum) kwa siku. Hii inakusaidia wewe kuweka malengo na faida unayoipata katika biashara yako.

Ni vizuri kuweka rekodi ya kila mauzo kwa maandishi ili kurahisisha tathmini yoyote inayoweza kufanywa kwa minajili ya kuboresha biashara.

7.Chunguza vitu wanavyopenda na vinavyowachukiza wateja wako
Ni rahisi kufahamu wateja wanapenda nini na wanachukia nini. Kwa upande wa vinywaji,ni wazi kuwa vile vinywaji vinavyowahi kuisha kuliko vingine ndivyo vinapendwa na wateja na inabidi viwepo vingi vya kutosha. Kuhusu ubora wa huduma, unaweza kuongea na wateja wako (wenye busara) moja kwa moja ili kutoa kero zao ili zile zinazorekebishika zirekebishwe maramoja ili kuepuka kupoteza wateja ambao ndio muhimiri wa biashara yako.

8.Epuka urafiki na mikopo kazini
Hii inawahusu wote, wewe mwenye bar, meneja na wahudumu. Biashara nyingi zinakufa au hazizai matunda tarajiwa kutokana na urafiki na mikopo mingi. Katika bar yako ni vema ifahamike kwa wote kuwa Ofa na mikopo isiyo na ulazima sio njia sahihi za uendeshaji wa biashara. Weka taratibu za wazi kuhusu kukata kwenye posho,malipo au mshahara ya mfanyakazi yeyote ambaye kwa uzembe wake mwenyewe au makusudi amesababisha upungufu katika mauzo ya kawaida ya kila siku.

9.Ubunifu na upekee katika biashara ya 'Bar' ni muhimu
Jitahidi kuwa na ubunifu wa pekee ili kufanya biashara yako kuwa tofauti na wengine. Kwa mfano, unaweza kuandaa tamasha dogo la muziki, urembo au vichekesho katika bar yako ambapo kiingilio chake ni kununua ki/vinywaji tu. Huu au ubunifu mwingine wowote utakukuzia biashara yako kwa kasi kubwa kama utakuwa makini kuwa utekelezaji wa ubunifu usigharimu zaidi ya faida unayoweza kupata.

10.Pokea ushauri na maoni kutoka kwa watu wengine
Unatakiwa kuacha masikio yako wazi kwa ajili ya kupokea kila wazo litakalolenga uboreshaji wa biashara yako wa Bar kutoka kwa wazoefu wa biashara ya namna hii au hata washauri wengine. Kuwa makini pia katika kutekeleza ushauri unaopewa kwani si wote wanaokupa uashauri wanakutakia mema katika mafanikio yako na wala si wote wanaokutakia mabaya katika biashara yako.

Hizo njia 10 zikifuatwa vizuri zitakusaidia sana katika biashara yako ya Bar.Kwa ushauri wowote, maswali au maoni kuhusu makala za blogu yetu yatatufikia kupitia barua pepe inamotoblog@gmail.com , namba ya simu +255764004963 au comment hapa chini. ASANTE na KARIBU TENA.

5 comments:

  1. Replies
    1. "
      525244a298Here are best materials for you!
      BEST VIDEO ABOUT HOW TO MAKE MONEY ONLINE:
      I found this is No1 video about how to make money online
      Hope that it help you more
      source: 12 ways to make money online in your lifetime







      Jennifer Lee Mar 21, 2018 at 7:36 PM
      LEARN FREE HOW TO MAKE MONEY ONLINE BY AFFILIATE MARKETING
      This is a free course by affilorama, the leading internet marketing academy,rated 4.7 * by 87k+ students.
      source: Free training affiliate marketing online







      John Smith Mar 23, 2018 at 8:36 PM
      LEARN HOW TO BECOME MILLIONAIRE ONLINE
      This is one of best online course about how to become millionaire online.
      It is difficult to become a millionaire, so perhaps this course is only rated 4.4*.
      source: How to become millionaire online in one year







      Juan Carlos Mar 27, 2018 at 8:36 PM
      12 SECRETS TO GET ANY GIRL TO LIKE YOU
      This is one of top secrets that help you get any girl to like you.
      Rated 4.7* by 5600+ students.
      Link: 12 secrets to get any girl to like you







      Mike Jones Mar 29, 2018 at 9:36 PM
      LEARN FREE PIANO ONLINE:
      This course is organized by LearnPianoIn30Days. This site offer 14 days free training for only $1.
      More details: $1 Trial to learn piano in 14 days







      David Smith April 1, 2018 at 10:36 PM
      13 SECRETS TO CAPTIVATE ANY MAN:
      This is one of top secrets that help you get any girl to like you.
      Rated 4.7* by 5600+ students.
      Link: 13 secrets to captivate any man







      David Hu April 2, 2018 at 10:36 PM
      LEARN FREE GUITAR ONLINE:
      This course is organized by LearnPianoIn30Days. This site offer 21 days free training for only $1.
      More details: Trial 1$ learn guitar online in 21 days







      Peter Ho April 3, 2018 at 14:36 PM
      DO YOU LOVE MAGIC?
      This is best course online about how to become a magician!
      This training course offer free trial and 60 days money back guarantee
      Link: Trial to Learn Mentalism Effects and Magic Tricks





      Jennifer Tran April 3, 2018 at 19:36 PM
      HOW TO LOSE 1 POUND OF BELLY FAT EVERY 72 HOURS?
      yes it can. Bruce Krahn and Dr. Heinrick created this program specifically for men and woman.
      The core of the program is a formula by Heinrick that is supposed to work well against belly fat and its associated health issues
      Here are link: Link: Secrets to lose 1 pound of belly fat every 72 hours





      "

      Delete
  2. asante nimeelewa na itnisaidia kupiga hatua,nafanya biashara ya grocery,je unaweza kunisaidi jinsi ya kupanga na kuweka vizuri mahesabu kwa siku,wiki na mwezi? maan hawa mabinti wanachanganya sana..ntashkru sana ukinisaidia.Kazi njema.kwa mawassiliano 0766120706 email aidanlulandala@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Awesome website! Your style is so fresh in comparison with most other people. Thanks for posting whenever you have the opportunity to, I will be sure to save your website! software companies in Chandigarh

    ReplyDelete