MTAJI
Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida. Biashara yoyote iwayo lazima ianze na mtaji. Kuna aina tano za mitaji kama ifuatavyo:-
1. Mtaji wa fedha( financial capital)
2. Binadamu mwenyewe( human capital) vitu kama ujuzi, elimu na kufanya kazi kwa bidii.
3. Jamii ( social network capital) ushirikiano na watu wengine katika biashara
4. utamaduni halisi wa mjasiliamali- utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii,historia ya familia
5. Fani au utaalamu katika jambo flani
JINSI YA KUPATA MTAJI.
Hapa
tunaangalia vyanzo vya mtaji kwa mjasiliamali. Wajasiliamali wengi
wanapata changamoto kubwa katika kupata mitaji ya kuanzishia biashara.
nivigumu kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji wa kutosha,hivyo basi
mtaji ni muhimu sana lakini mtaji pekeyake hautoshi kuanzisha biashara
ni lazima uwe na elimu ya ujasiliamali ili uweze kufanikiwa katika
biashara. kuna njia mbalimbali za kupata mtaji na njia hizo
zimegawanyika katika mafungu mawili ambayo ni chanzo cha ndani na chanzo
cha nje.
Chanzo cha ndani ( internal sources of capital)
1. Mtaji toka
kwa mjasiliamali mwenyewe. Huu ni mtaji ambao mjasiliamali anakuwanao
kabla hajaanza biashara. huu ni mtaji bora sana kwani humilikiwa na
mjasiliamali mwenyewe na hatakiwi kurudisha rejesho hata baada ya kupata
faida.
2. Mtaji ambao
unapatikana wakati biashara injiendesha. Faida inayopatikana katika
biashara inaweza kutumika kama mtaji. njia hii ndio huchangia kukua kwa
biashara.
3. hisa. baadhi
yawajasiliamali wanaweza kuamua kuwekeza katika hisa za makampuni. Uwekezaji katika hisa husaidia kupata mtaji pale ambapo kampuni litagawa
faida kwa wanachama waliowekeza katika hisa. pia mjasiliamali anaweza
kupata mtaji kwa kuuza hisa kwa mtu mwingine au muwekezaji wa nje.
chanzo cha nje ( external sources of capital)
Hapa
tunaangalia mtaji ambao mjasiliamali anaweza kuupata toka nje ya yeye
mwenyewe. Baadhi ya vyanzo hivyo ni kama ifuatavyo.
1. Mkopo toka benki
huu ni mkopo
ambao ulipaji wake ni wa muda mrefu.viwango vyariba si vikubwa sana
ambavyo mjasiliamali anaweza kumudu kulipa endapo biashara itafanikiwa.
mikopo ya benki inahitaji dhamana ya vitu visivyo hamishika mfano
nyumba, shamba nk.
2.Mkopo toka SACCOS
3.Mkopo (kwa riba) kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa.
0 comments:
Post a Comment