Wednesday 18 December 2013

JIELIMISHE KWA KIFUPI KUHUSU 'SMARTPHONES'




     Smartphones ni aina ya simu zinazojizolea idadi kubwa ya watumiaji siku hadi siku hapa kwetu Tanzania.
   Watumiaji wengi hufurahishwa na jinsi zinavyofanya kazi kwa ustadi na mbwe mbwe nyingi.
    Unaweza ukajiuliza ni programu gani iliyo ndani ya hizi simu inayoziendesha programu za maombi(Application program) ambazo zote hukaa juu yake kuweza kufanya vitu vyote hivyo.

Kampuni mbalimbali zinazotengeneza smartphones kama Nokia, Samsung, Google na Apple kila moja inatumia programu endeshi(Operating System kwa kifupi OS) tofauti.
      Hebu leo tujuzane kwa kifupi aina hizo za programu endeshi(Operating System) na kampuni zinazozitumia.

1.SYMBIAN

   Asili yake ni Japan na ilianzishwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Nokia, Sony na nyingine ambazo si maarufu. Hii ni programu endeshi(Operating System) inayoongoza kwa kutumiwa na vifaa vingi zaidi duniani kuliko programu endeshi(OS) nyingine kwasababu vifaa vinavyoitumia vimesambaa sana.
   Kwa hiyo yeyote anayetumia smartphone ya Nokia ajue ndani yake inatumia programu endeshi inayoitwa Symbian.

2.RIM(Research In Motion) OS au BLACKBERRY OS

Programu endeshi hii iliasisiwa huko Canada na iliundwa kwa ajili ya kutumika kwenye kompyuta za mkono za BlackBerry.
Kwa hiyo mtumiaji yeyote wa simu aina ya BlackBerry ajue ndani yake kuna programu endeshi ya RIM OS.

3.iPHONE OS
   Hii ilitengenezwa na kampuni ya Apple ili kuendesha vifaa vyake vya iPhone, iPod Touch na iPad.
   Kwasasa ndiyo kampuni ambayo matumizi yake yanakuwa kwa kasi sana.
Kwahiyo yeyote anayetumia smartphone ya Apple ajue ndani yake kuna programu endeshi inayoitwa iPhone OS.

4. ANDROID
    Ilitengenezwa na kampuni inayoitwa Android Inc. na baadaye kampuni ya Google ikapendezwa nayo na ikainunua hii programu endeshi na kuitumia katika smartphone zake.
   Kwahiyo yeyote anayetumia smartphone ya Google ajue ndani yake kuna programu endeshi ya Android.

5.WINDOWS PHONE OS
   Programu endeshi(Windows phone OS) ilitengenezwa na kampuni ya Microsoft na ilibuniwa kwa ajili ya kuwezesha uundaji wa mtandao wa kijamii na ujumbe wa papo kwa papo baina ya watumiaji.
     Kwa anayetumia smartphone kama za Samsung Galaxy S III ajue ndani yake kuna programu endeshi ya Windows phone OS.


1 comments:

  1. I am convinced of your point, where you said that it is tough to hiring a remote developer at a low cost. For full-time, it is always expensive, but you can hire freelancers who work according to hourly pay or charge according to per app. I know one freelancing platform that is Eiliana.com. You can take help from there.

    ReplyDelete