Sunday, 17 November 2013

JINSI YA KUFANYA UJASIRIAMALI KUWA KAZI YENYE MAFANIKIO MAKUBWA.


(Pichani, ni mjasiriamali maarufu Tanzania na mwandishi wa vitabu, Eric Shigongo)

Ujasiriamali kuwa kazi, hapa nalenga kuonyesha ni jinsi gani mtu anaweza kujiajiri kama mjasiriamali na kuachana na mawazo ya kuajiriwa. Kuwa na mtaji pekee haitoshi ili mtu aweze kujiajiri bali mjasiriamali anahitaji kujua na kuvifanyia kazi vitu vifuatavyo ambavyo ni jinsi ya kupata wazo la biashara,kugundua na kutambua biashara sahihi,vigezo muhimu wakati wa kuchagua biahara ya kufanya,vitu muhimu vya kufuata wakati wa kuanzisha biashara na kazi za mjasiriamali.

Kabla hujanzisha biashara jiulize maswali yafuatayo
  •       Kwanini unataka kuanzisha biashara?
  •       Je upo tayari kufanya biashara?
  •       Je unamalengo gani katika biashara hiyo?
  •       Je unaujuzi na elimu ya  kutosha katika kunzisha,kuendesha    na kukua kibiashara?
  •       Mtaji kiasi gani unahitajika ili kuanzisha biashara?
  •       Biashara ya pekeyako au ya ushirikiano?

Jinsi ya kupata wazo la biashara

  •   Tafuta msaada toka kwa wote ambao wapo katika biashara,watakwambia vitu muhimu katika biashara.
  •   Angalia wengine wanafanya nini, tambua matatizo wanayokumbana nayo na kisha fikiri njia sahihi za kutatua matatizo hayo.
  •  Jadiri pamoja na marafiki na jamaa wa karibu juu ya kile unchotaka kufanya
  •  Kuwa mdadisi kwa kuchunguza vitu kwa makini,tembelea maeneo mengine ili kujua wanafanya nini
  •   Fikiri kufanya kiu kipya ambacho hakijafanywa katika eneo ulilopo

Faida za kuwa na wazo la biashara

  1.  Hupunguza vikwaazo katika kuendesha biashara
  2.     Husaidia katika kufanya maamuzi sahihi ya biashara gani uanzishe
  3.    Kupata mafanikia katika biashara
  4.     Ni hamasa kubwa katika kuingia katika biashara

Jinsi kuugundua na kutambua biashara sahihi

  •  Kuwa makini katika kuchaga aina ya biashara ya kufanya
  • chagua kulingana na uwezo wako katika kuendesha biashara hiyo
  •  chagua biashara unayo ipenda kwani uwezekano wa kuifanya vizuri ni mkubwa
  • amua biashara ya kufanya hasa bada ya kufanya uchunguzi wa kutosha na kutafuta habari za kina juu ya biashara husika hi itakusaidia kufanya biashara bilia vikwazo vingi

vigezo muhimu wakati wa kuchagua biashara ya kufanya

  • uwezekano wa kufanikiwa
  • faida itakayopatikana
  • kutambua vikwazo katika bishara
  • biashara inayo vutia
  • elimu ya biashara pamoja na rasilimali watu
  • mtaji
  • masoko
  • upatikanaji wa stoo za kuhifadhia bidhaa
  • upatikanaji wa malighafi
  • usafiri
  • uwezekano wa kupata msaada toka serikalini

kazi ya mjasiliamali

  1.      kuaandaa mpango wa biashara
  2.       kuatafuta mtaji
  3.      kupanga bei
  4.       kutunza kumbukumbu za biashara
  5.      kutunza fedha
  6.       kujitegemea
  7.     kuchanganua gharama
  8.      kutangaza bidhaa anazouza (Kutafuta soko)
  9.      kubaini vikwazo katika biashara
  10.     ubunifu



 Ufunguo wa mafanikio katika ujasiliamali 

Mpango  biashara

kabla hujaanza biashara hakikisha unaandaa/kuandika mpango biashara madhubuti ambao utaeleza kipi utafanya na mpangilio mzima wa biashara yako. Pia fikiri kuhusu kesho, wiki ijayo na tazama mbele zaidi

dondoo

  •  tambua mambo yanaenda yakibadilika hivyo nawe badilika kulingana na wakati pamoja na mazingira
  •  tambua kuwa huwezi fanya kila kitu ukiwa pekeyako
  •   mjasiliamali mzuri ni yule anaye  fikiri na kutazama mbele (future oriented)
  •   mjasiriamali mzuri ni yule anayetumia muda vizuri
  •   mpango biashara utakusidia kuona fulsa mpya na chagamoto mbalimbali katika biashara zako
  •   tafuta ushauri toka kwa wataalamu mbalimbali wa biashara na ujasiliamali kwa kile unacho kifanya
  •   uthubutu ni ufunguo wa mafanikio katika ujasiliamali.

Jinsi ya kupata mafanikio katika biashara

Kunanjia nyingi unaweza kuzitumia ili kufikia mafanikio katiaka biashara, baadhi ni kama zifuatazo.
Fikiri kuhusu……

  1.   jinsi ya kubadiri wazo la biashara na kuwa biashara
  2. imarisha na ongeza ubora wa bidhaa na huduma unazotoa
  3. gundua,tambua na anzisha bidhaa mpya na huduma
  4. jinsi ya kuvutia wateja
  5. namna ya kusimamia biashara yako hata kama haupo (weka wasaidizi)
  6. kuongeza juhudi
  7. kuajiri wasaidizi bora

jitofautishe katika utoaji wa huduma na bidhaa

kwanini wateja waje kwako?

Kujitofautisha katika kuuza bidhaa na aina ya huduma unayotoa ni kitu muhimu sana. Hii itasababisha wateja wengi wafuate huduma zako,wafanyabiashara wengi wanaamini kuwa kupunguza bei ni kivutio kikubwa cha wateja katika biashara, lakini sio bei tu ianayoweza kuvutia wateja wengi katika huduma zako, wateja wengi huthamini huduma bora na bidhaa bora kama ifuatavyo….
  •    Ubora wa bidhaa yenyewe na huduma unazo toa
  •    Urahisi wakupata huduma na bidhaa zako
  •    Upatikanaji wa bidhaa na huduma katika muda muafaka.
  •    Usalama wa bidhaa na huduma zako.
  •    Kupendelea kuuza bidhaa zisizoharibu mazingira.
  •    Sehemu zilipozalishwa bidhaa. (nchini au ughaibuni mf. China)
  •    Kuzingatia Maoni  ya wateja wako juu ya bidhaa na huduma unazotoa.
  •   Ubunifu wa  Kila siku na matumizi ya njia mbali mbali ambazo zinafanya wateja wapende bidhaa zako zaidi.

1 comments: