Wednesday, 11 December 2013

Jinsi Ya Kuandika Andiko La Mradi



Je unahitaji huduma ya Jinsi Ya Kuandika Andiko La Mradi?

Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa kitaasisi na kifedha
  1. Mradi huo unaitwaje?, Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
  2. Maswali mengine ni kama ifuatavyo; Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo lilianza nkwa nani?
  3. Kwanini tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki?, Je, mradi ni suluhisho halisi na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
  4. Unaweza kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje katika jamii hii.
  5. Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?
  6. Malengo au Lengo kuu la mradi ninini? Madhumuni yake mengine ni yapi? Shughuli za mradi na majukumu madogomadogo ninini? Ambayo lazima yapangwe kimantiki na kwa matarajio yenye kufikia lengo.
  7. Ni wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu, mchango wa wadau hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu ?
  8. Kuna uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala la mazingira linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na magonjwa yasiyotibika yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa mradi huu?
  9. Umepanga kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi huu? Uendelevu wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu kwa namna gani?
  10. Swali lingine ni kama kuna mradi kama huu uliowahi kutekelezwa hapo au jirani na hapo katika kipindi kifupi kilichopita.
NB: Maswali haya yakijibiwa vizuri kwa mtiririko sahihi huitwa andiko la mrad.

0 comments:

Post a Comment