Wednesday, 11 December 2013

Masharti Tano (5) Muhimu Katika Kupata Mkopo wa Benki





1.       Je ni biashara mpya au inayoendelea?
Biashara inayoendelea na yenye angalau miaka mitatu ina nafasi kubwa kuliko zile changa au mpya

2.       Aina ya biashara unayofanya
Biashara za kuzalisha zinanafasi kubwa kuliko zile za huduma au uchuuzi

3.       Integrity (historia safi )ya mkopaji
Historia safi ya mkopaji ya kukopa na kurudisha bila usumbufu inaongeza uwezekano mkubwa wa kupewa mkopo

4.       Dhamana na mdhamini wa mkopaji kama akishindwa kurudisha
Kwa bahati mbaya mkopaji akishindwa kurudisha kwa namna yeyote ile mkopo, je kitu gani kitafidia huo mkopo ili benki wasipate hasara AU nani atasimama kama mdhamini ili yeye ndie ashikwe endapo mkopaji atashindwa kurudisha mkopo. Aina ya dhamana na mdhamini atakayekubaliwa na benki itasaidia wewe kupata mkopo


5.     Mchanganuo wa Biashara
Mchanganuo wa biashara wenye kuonyesha mchanganuo wa kisekta, ushindani, uzalishaji, uongozi/utawala, masoko na mambo ya fedha (kwenye fedha hasa mtaji utakaohitajika, makisio ya mauzo, gharama, na faida. pia makisio ya balance sheet na cashflow itatakiwa pamoja na uwiano wa sehemu muhimu za biashara kama uwiano wa mauzo na matumizi, mauzo na mishahara, mauzo na mtaji, mauzoi na gharama ghafi, muda wa kurudisha gharama na kuanza kupata faida nk)

0 comments:

Post a Comment