Katika makala haya
tutakuletea uchambuzi wa wajasiliamali wenye mafanikio Afrika Mashariki
historia yao kimaisha, kiwango chao cha elimu, tabia binafsi, maadili na kanuni
wanazozishikilia, nidhamu, utajili wanaomiliki, mahusiano na maisha ya
kifamilia. Vilevile tutaangalia namna walivyo jenga biashara imara, namna
wanavyokabiliana na changa moto mbalimbali, mchango wao katika jamii, mawazo,
maoni na ushauri wao kwa wajasiliamali wanaochipukia.
Katika toleo hili tunakuletea mjasiliamali mwenye mafanikio afrika ya mashariki ambaye alianza na biashara ya mabaki ya mazao ya baharini, kushona viatu, biashara ya viazi na baadae mgahawa. Leo hii ni milionea anayemiliki rasilimali mbalimbali za viwanda, pamoja na vyombo vya usafiri ndani na nje ya nchi. M jasiliamali huyu si mwingine bali ni Said Salim Awadh Bakhresa.
Said Salim Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 mjini Zanzibar, alisoma elimu ya msingi hadi alipofikia umri wa miaka 14 ambapo aliacha shule kutokana na maisha ya familia kuwa magumu hivyo kujiingiza katika biashara ili aweze kuhudumia familia katika mahitaji kama chakula baada ya baba yake kukabiliwa na madeni.
Katika miaka ya 1960, wakati
Tanzania ilipokuwa nchi ya kijamaa na Kenya ikifuata siasa za kibepari,
Bakhresa aliweza kununua mabaki ya mazao ya baharini kama, mifupa na magamba ya
viumbe wa baharini na kuyauza Mombasa. Kutokana na tofauti ya kifedha
iliyokuwapo wakati huo, aliweza kununua ngozi za viatu kutoka Kenya na
kuzitumia kushonea viatu hapa Tanzania.Badae alifanya biashara ya viazi, mikate
na ice cream. K atika miaka ya 1970,s Bakhresa alifungua na kuendesha biashara
ya mgahawa. M gahawa huu alinunua kutoka kwa mgeni wa kihindi ukiwa na jina la
AZAM,jina ambalo analitumia kama nembo(brand) ya bidhaa zake kwa sasa. K atika
miaka ya 1990 s alinza uwekezaji katika viwanda.
Kwa sasa kiasi kikubwa cha
mchele na bidhaa za nafaka zinatoka katika kampuni ya Bakhresa Group iliyopo
kipawa (flour Mill) .Nchi jirani ya Rwanda kwa mfano, inategemea tani 120,000
za unga wa wangano kwa mwaka kutoka kwa kampuni ya Bakhresa.
Said Salim Awadh Bakhresa ni mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, ni Mtanzania anayemilki viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa za vyakula zinazouzika ndani na nje ya nchi. P ia kokote jijini Dar-es- salaam na mikoani, bidhaa za AZAM utasikia zikitajwa. Azam ni nembo(brand) ya bidhaa zinazotengenezwa kupitia makampuni ya Bakhresa, Azam ni neno la kihindi linalomaananisha ukubwa.
Bakhresa amejijengea jina
kibiashara kwani si ajabu kusikia watu wakisema, Amka na Azam, shinda na Azam
au sheherekea na Azam. Tafasili yake ni kwamba katika maisha yetu ya kila siku,
tunatumia bidhaa za Azam kwa kiasi kikubwa sana. Asubuhi tuamkapo tunapata
kifungua kinywa kwa vitafunwa vya Azam. M chana tunakula ugali, wali, au chips
na tunakunywa maji na juice kutoka Azam. J ioni kama utakula tambi au kunywa
soda n.k . u naweza kujikuta bado unatumia bidhaa za Azam. Hivyo ndivyo wimbo
wa bidhaa za Azam unavyo imbwa katika maisha ya Watanzania kila siku.
Kulingana na jarida la forbes Bakhresa ndiye anayeaminika kuwa tajiri namba moja nchini Tanzania, akishikilia nafasi ya 30 ya matajiri Afrika. M apato yake kwa mwaka ni zaidi ya dola za Kimarekani $520 milioni. Bakhresa ana wafanyakazi zaidi ya 2,000 wenye ajira rasmi.
Bakhresa ni mtu mashuhuri katika harakati za mapinduzi na maendeleo ya viwanda Tanzania Bara na Visiwani. jasiliamali huyu ameweza kujizolea sifa kemkem ndani na nje ya nchi, si tu kutokana na wingi wa bidhaa zake bali pia ni kutokana na bidhaa zake kukidhi viwango vya ubora kimataifa.
Mjasiliamali huyu amejijengea umaarufu mkubwa katika biashara kwa takribani miongo mitatu sasa. Ameweza kujenga timu imara ambayo inasimamiwa na wakurugenzi makini ambao ni watoto wake mwenyewe. Bakhresa Group ina matawi katika nchi sita ambazo ni,. Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Amejikita zaidi katika usindikaji wa vyakula. Ana viwanda vya kusaga unga wa ngano na mahindi, viwanda vya ukoboaji wa mchele, uandaaji wa vyakula kama mikate,chapatti, vinywaji kama maji (Uhai) , juisi za matunda na soda, pamoja na ice cream. Pia ana kiwanda cha vifungashio vya bidhaa mbalimbali, biashara ya mafuta ya magari na mitambo. Vilevile anazo boti za usafilishaji abiria ambazo hufanya safari zake katika Bahari ya Hindi. Hali kadhalika, anafanya biashara ya usafirishaji mizigo (azam logistics). Katika michezo ,Bakhresa anamiliki timu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la Azam Footbal Club ambayo imefikia kiwango cha kucheza ligi kuu Tanzania bara.
Unapomzungumzia Said Salim Bakhresa unamzungumzia mtu wa aina yake katika Tanzania, ni mtu anayesemkana kusimamia maono yake na kuhakikisha yanatimilika kikamilifu. Anauzoefu mkubwa katika usimamizi wa biashara , ni mtu anaye fanya tafiti juu ya maendeleo ya viwanda na masoko katika kutambua mahitaji ya watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Anatumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha bidhaa zake zinaliteka soko la ndani na la nje ya nchi. Licha ya kutangaza bidhaa zake kupitia redio na televisheni, anapata fursa ya kujitangaza kupitia timu yake ya mpira wa miguu anayoimiliki(Azam Football Club) hivyo anatangaza bidhaa zake kupitia michezo. Vilevile anawatumia wachuuzi au Machinga katika kutangaza bidhaa zake mfano Ice cream. Pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo , mfano kumiliki na kuendesha biashara mbalimbali ndani na nje ya nchi , bado kuna vikwazo na changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo ili kufikia malengo yake. Kwa mfano sera za biashara zisizosimamiwa vizuri katika ushindani wa masoko, gharama za teknolojia katika uzalishaji n.k.
Katika suala zima la kupanga , kudhubutu na kufanya ni vitu vya msingi katika kufikia mafanikio. Bakhresa ni mtu anayehamasisha Watanzania wasiogope kujifunza kwa vitendo, kwani wengi huhofia changamoto zinazoweza kusababisha, anguko katika biashara lakini mjasiliamali anapaswa kujiamini katika mawazo yake na kujiwekea mipango mathubuti. Ka zi ya ujasiliamali inahitaji ubunifu kwa kiasi kikubwa katika kuweza kubaini na kuibua fursa zilizopo na hata kuweza kukabiliana na changamoto zake.
Kwa sasa bado Bakhresa anaendelea kutanua wigo wa biashara katika kuweza kufikia nchi nyingi zaidi duniani. Hata hivyo anaamini kwamba bidhaa zake bado hazijatosheleza soko la ndani . Bado anazitizama fursa zilizopo katika soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Hivyo basi anajitahidi katika kuboresha bidhaa zake zaidi ili kuhakikisha zinakuwa na ubora unaotakiwa na hatimaye kushikilia soko la kitaifa na kimataifa.
Pia anatoa ushauri kwa Watanzania, hususani vijana, wajitahidi kufikiri vizuri na kutazama fursa zilizopo nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawainua wao kiuchumi , ili hatimaye kuondokana na umaskini unaolikabili taifa letu.
Chanzo cha habari Gazeti la Nguzo yangu.
Tumekuletea habari hii ya Bwana BAKHRESA ili uone kuwa
huhitaji mtaji mkubwa kuwa Tajiri, unaweza kuanza taratibu taratibu nawe
utafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment