Ulishaji:
Kuku wa kienyeji
wanaweza kulishwa
kwa kutumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika
sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.
sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.
Banda::
Kuku wawe wa kienyeji
au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda.
Wanahitaji chumba chenye
nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini. Maji ya kunywa: Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na
kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.

Chanjo kwa mifugo ni
lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile
Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida
hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.
Uwekaji wa kumbukumbu:
Kumbukumbu zijumuishe
aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji,
muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.
muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.
Mwanzoni unahitaji nini?
Wafugaji walio wengi
wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa
ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga. Ni busara kuwa na
vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku
bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika
kwa ajili ya vifaranga 200;
• Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima
ukamilishwe.
• Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.
0 comments:
Post a Comment