Wednesday 11 December 2013

Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo



Je unahitaji huduma ya Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo?

Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo ni mtaji tosha wa kukuwezesha kuanzisha biashara. Hatua ya kwanza ikiwa imebeba hatua zote kwani biashara inahitaji utayari (kuamua) zaidi ya vitu vingine kama mtaji nk
  1. Hatua ya kuamua kuingia katika biashara
Kuamua kuingia katika biashara ni majumuisho ya utayari wa kisaikolojia, kiakili, kiuchumi na kukabiliana na hatari au vitisho vyote vitakavyojitokeza kwenye biashara


  1. Hatua ya kuchanganua uwezo na udhaifu wako
Maeneo manne ni muhimu yapatiwe taarifa halisi na kuchukua hatua ili uweze kumudu kufanya biashara husika

Mazingira wezeshi
Mazingira pingamizi
Mazingira ya Ndani
Uwezo
Uwezo wako katika kuendesha biashara mfano: utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
Udhaifu
Udhaifu wako katika kuendesha biashara mfano: ukosefu wa utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
Mazingira ya Nje
Fursa
Kuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio wa jamii nk
Vitisho
Kutokuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio mbaya wa jamii nk

  1. Hatua ya kupata mafunzo
Baada ya kujua udhaifu wako, pata mafunzo
Mfano:- Ya kupata ufundi au kubadili mitizamo
Kupata utaalam wa kiufundi katika biashara husika

  1. Hatua ya kupeleleza mazingira utakayofanya biashara ili kujua:
           i)       Fursa nzuri zilizopo
           ii)      Vitisho au hatari zitakazoikabili biashara yako (vihatarishi vya biashara                                              husika kama vile sera mbovu, barabara mbovu, hali ya hewa mbovu nk)
  1. Hatua ya kuchagua biashara gani ufanye
i)             Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)
ii)            Kuuza bidhaa (Trading)
iii)          Kutoa huduma (Service)


·         Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)
Kutengeneza bidhaa ni kutumia rasilimali watu na malighafi ili kutengeneza bidhaa ya kuuza kwa mlaji au mchuuzi. Bidhaa ni kama vyakula, vyombo, nk

·         Kuuza bidhaa (Trading)
Kuchuuza bidhaa zilizotengenezwa hapo juu no. A(a)

·         Kutoa huduma (Service)
Kutumia ujuzi wako au wa wengine katika kuwahudumia watu na shida zao kwa malipo. Mfano kufundisha, kutibu, kusafirisha, kutumbuiza nk

  1. Hatua ya utafiti wa soko (Market Survey)
i)             Ukubwa wa soko
ii)            Mgawanyo wa soko
iii)          Aina ya soko/masoko
iv)          NK

  1. Kuamua aina ya mfumo wa biashara utakayofanya
Fuatilia maelezo ya kila mfumo ukitilia maanani faida na hasara za kila mfumo. Unaweza pia kumtumia mshauri wa masuala ya biashara kukushauri kulingana na mazingira yako utakayofanyia biashara.
         i)  Mtu mmoja (sole proprietor)
·         Faida yake
         -Kuanzisha ni rahisi
         -Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu

·         Hasara yake
         -Biashara ikipata shida mmiliki anahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
        ii) Ushirika (>watu wawili) (partnership)
·         Faida yake
-Kuanzisha ni rahisi
-Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu

·         Hasara yake
-Biashara ikipata shida wamiliki wanahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
-Mikataba inayoingiwa na mmoja wa washirika huwabana na wengine wasiohusika
        iii)  Kampuni ya umma au mashirika ya umma (public companies)(zaidi ya watu wawili bila kikomo)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Ni rahisi kuvutia mitaji mikubwa kupitia masoko ya hisa
Hasara yake
Haina usiri hivyo ni hatari kwani washindani wa biashara husika wanaweza kutumia taarifa hizo kujipanga
Muda na rasilimali muda kupotea kwa shughuli za kihasibu na kazi za makaratasi
iv)          Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa hisa (private companies limited by shares) (watu wawili hadi 50)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Hasara yake
Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

v)   Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa udhamini (private companies limited by guarantees) (watu wawili hadi 50)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Hasara yake
Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka
vi)          Jumuiya (association)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
vii)         Vyama vya ushirika
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
viii)        Mashirika yasiyo ya kiserikali
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
  • Ukishachagua mfumo mzuri wa biashara yako, unatakiwa kuanza mchakato wa kuisajili katika mamlaka ya usajili wa makampuni inayoitwa BRELA ambayo ofisi zake zipo Jengo la shirika –Dar es salaam
  1. Hatua ya kuchagua sehemu ya biashara
i)             Kama ni sheli itabidi iwekwe kando ya barabara yenye magari mengi
  1. Hatua ya  kuchagua technolojia
i)             Teknolojia itasaidia kujua
a)    Aina ya  watumishi
b)   Aina ya vitendea kazi mashine  /mitambo
Mfano kilimo cha maksai na kukamua kwa mashine
ii)            Teknolojia nzuri ni lazima iwe na sifa zifuatazo
a)    Ni rahisi kutumiwa
b)   Iwe rahisi kupata msaada kama mafundi nk
c)    Iwe inaendana na tamaduni husika
d)   Iwe ni rafiki wa watu na mazingira
e)    Iwe na gharama ndogo za uendeshaji
f)     Inaendelezeka
  1. Hatua ya  kununua mashine na vifaa
Mashine na mitambo mingine itategemea sana uchaguzi wa teknolojia hapo juu 8(i)
Mashine zote na mitambo ni lazima kuzingatia yaliyotajwa hapo juu 8(ii)
  1. Hatua ya usajili wa biashara
i)              Hii hufanywa mara nyingi kwenye manispaa husika. Leseni kwa wafanya biashara ndogondogo ni bure (biashara ndogondogo ni ile ambayo mauzo yake hayazidi Shs 20 milioni kwa mwaka)

  1. Hatua ya kuandika Mchanganuo wa Biashara (Business Plan)
  • Baada ya kufanya hayo yote sasa ni wakati mzuri wa kuandika  mchanganuo wa biashara yako
  • Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biahara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki
Mambo muhimu ya kujua katika kuandika Mchanganuo wa Biashara
  1. Muhtasari wa biashara yako
  2. Historia na maelezo ya biashara yako
  3. Maelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yako
  4. Mchanganuo wa masoko
    1. Ukubwa wa soko
    2. Mgawanyo wa soko
    3. Aina ya soko/masoko
    4. Mchanganuo wa ushindani
      1. Watoa huduma au wauza bidhaa kama yako
      2. Udhaifu wao
      3. Uwezo wao
      4. Mkakati wa utekelezaji
        1. Uongozi na usimamizi wa kazi
        2. Uchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yako
        3. Mkakati wa Uzalishaji
        4. Mkakati wa kuuza
  1. Mpango wa fedha
    1. Uchambuzi wa mahitaji ya mtaji
    2. Wapi utatoa mtaji
    3. Matumizi ya mtaji
    4. Makisio ya Mauzo
    5. Uchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)
    6. Makisio ya faida au hasara
    7. Makisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)
    8. Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)
    9. Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)
    10. Viambatanisho
      i.    Lesseni
      ii.    Cheti cha ulipaji kodi
      iii.    Cheti cha usajili
      iv.    Taarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu
      v.    nk
  1. Hatua ya  kupanga juu ya pesa.
Kutafuta mikopo kwa kufuata utaratibu wa taasisi za fedha husika
Taasisi nyingi huhitaji yafuatayo
  1. Dhamana ya mkopo
  2. Uzoefu wa biashara husika
  3. Mchanganuo wa biashara
  4. Maombi ya mkopo
  1. Hatua ya ufahamu wa kiufundi.
Hii ifanywe ili mwenye biashara apate ufahamu wa kiufundi juu ya biashara yake hasa kutoka kwa taasisi husika au mshauri wa biashara (consultant).
  1. Hatua ya kujua vyanzo vya nishati:
Kama ni umeme hakikisha iko sawa na umeme utakidhi matakwa ya biashara.
Kama ni mafuta uhakikishe mafuta inapatikana na bei haitaadhiri bei ya bidhaa
  1. Hatua ya kuweka vifaa: (Machines installation)
Wataalam husika wafanye hii kazi
  1. Hatua ya kuajiri wafanyakazi.
Wafanyakazi wako wengi mtaani, lakini kumpata mtu atakayekidhi matakwa ya biashara yako kwa maana ya ubora na kufikia lengo la uzalishaji inahitaji usambazaji wa taarifa kwa upana zaidi na kwa maeneo maalum ambayo unategemea wafanyakazi watoke. Mfano vyuoni, makanisani nk
Unashauriwa pia kutumia marafiki na ndugu wa karibu ili upate mfanyakazi ambaye ni bora zaidi
  1. Hatua ya  kujua upatikanaji wa malighafi
Malighafi bila ubishi ni kiungo muhimu kwa biashara yeyote inayohusisha bidhaa. Vyanzo vya kupata malighafi ni muhimu ijulikane na iwe ya uhakika.
  1. Hatua ya uzalishaji mali
i)             Uzalishaji wa majaribio , Kuuza kwa majaribio kutoa huduma kwa majaribio muda – miezi 2-6, nk
ii)            Kuanza biashara rasmi
  1. Hatua ya kuhakikisha bidhaa yako hainakiliki
i)             Kutunza siri ya unavyozalisha au kutoa huduma tofauti na wengine
ii)            Tunza vizuri siri zingine za biashara yako
  1. Usalama wa biashara yako
i)              Epuka majengo ambayo ni rahisi kuwaka moto, kubomolewa na wezi, wizi katika pesa za mauzo, utapeli wa bidhaa katika kununua na kuuza nk.
  1. Hatua ya kuuza (Selling)
-                      Kufikia wateja (fikiria utamfikiaje mteja wako wa kwanza – maelezo zaidi yatakuwepo katika mchanganuo wa biashara)
-                      Kusambasa huduma/bidhaa
-                      Kuweka bei
-                      Kutangazia biashara
-                      Promosheni nk.
  1. Hatua ya Utafiti wa soko (Market Research)
-                      Hii ifanywe kila mara ili kujua kama wateja wamebadilika au bado Ili kujua kama wanapenda huduma/bidhaa zako au la.
-                      Kujua biashara yako imekamata asilimia gani katika soko
-                      Kupata maoni ya wateja ili kuboresha biashara/huduma/bidhaa
Namna ya kufanya utafiti
i)            Utafiti wa kuendelea
Kila mteja anaponunua bidhaa, ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
ii)           Utafiti maalum
Huu ufanywe wakati wa kutoa vivutiuo maalum au promosheni maalum.
Mteja wa promosheni ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
  1. Hatua ya kusimamia na kuthibiti biashara: 
Hii ni kuhakikisha kuwa biashara inakwenda kama ilivyobuniwa /pangwa.
  1. Hatua ya kutathmini biashara. 
Hii ni kujua kama biashara imekwenda kama ilivyobuniwa /pangwa.
Mambo ya kuangalia
  1. Mapato na matumizi
  2. Bajeti iliyiopita
  3. Matokeo ya utaifit/wa soko
  1. Hatua ya kufanya maboresho/mabadiliko
Unaweza kumuajiri au kumtumia mtaalam wa sekta hiyo kufanya taadhmini ya biashara yako.
Fanya sawa sawa na matokeo ya tathmini/utafiti

0 comments:

Post a Comment