1.
Je ni biashara mpya au inayoendelea?
Biashara
inayoendelea na yenye angalau miaka mitatu ina nafasi kubwa kuliko zile changa
au mpya
2.
Aina ya biashara unayofanya
Biashara za
kuzalisha zinanafasi kubwa kuliko zile za huduma au uchuuzi
3.
Integrity (historia safi )ya mkopaji
Historia safi ya
mkopaji ya kukopa na kurudisha bila usumbufu inaongeza uwezekano mkubwa wa
kupewa mkopo
4.
Dhamana na mdhamini wa mkopaji kama akishindwa kurudisha
Kwa bahati mbaya
mkopaji akishindwa kurudisha kwa namna yeyote ile mkopo, je kitu gani kitafidia
huo mkopo ili benki wasipate hasara AU nani atasimama kama mdhamini ili yeye
ndie ashikwe endapo mkopaji atashindwa kurudisha mkopo. Aina ya dhamana na
mdhamini atakayekubaliwa na benki itasaidia wewe kupata mkopo
5.
Mchanganuo wa Biashara
Mchanganuo wa
biashara wenye kuonyesha mchanganuo wa kisekta, ushindani, uzalishaji,
uongozi/utawala, masoko na mambo ya fedha (kwenye fedha hasa mtaji
utakaohitajika, makisio ya mauzo, gharama, na faida. pia makisio ya balance sheet
na cashflow itatakiwa pamoja na uwiano wa sehemu muhimu za biashara kama uwiano
wa mauzo na matumizi, mauzo na mishahara, mauzo na mtaji, mauzoi na gharama
ghafi, muda wa kurudisha gharama na kuanza kupata faida nk)
0 comments:
Post a Comment