Rangi inachukua nafasi kubwa sana katika kuchochea hali au tabia ya mtu au watu siku hadi siku.Rangi inachukua nafasi kubwa sana katika maana ya mambo hapa duniani kutoka kwa watu unaokutana nao au wewe mwenyewe,rangi inachukua nafasi ya kukutabiria wewe nini unataka kiwe ili ufanikiwe au lah!,haijalishi kama wewe unajua maana ujumbe ya rangi uliovaa au hujui(imetoke kwa kutokujua)dunia inakupatia kile ulicho wasiliana nacho kwa njia ya rangi. Tafiti nyingi moja wapo hii ya CCICOLOR - Institute for Colour Researchs inasema kuwa watu hufanya maamuzi ndani ya akili iliyofichika(subconscious mind) kuhusiana na mazingira au bidhaa ndani ya sekunde 90 toka kukitizama kitu au mazingira na kati ya 62% na 90% ya ukaguzi au maamuzi haya yanatokana na aina ya rangi pekee.Tafiti nyingine zinasema 92% inaaminika rangu huwasilisha(hutoa ujumbe kwa watu) picha ya ubora wa bidhaa a,na Asilimia 90% rangi hutumika kuwavuta wateja wapya na asilimia 83% huwawezesha watu kukumbuka kitu kama rangi ikitumika hizi tafiti zote zimefanywa na Xerox corporation na International communication research kutoka mwaka 2003 februari.Nimeshuhudia mara nyingi watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika mambo mbalimbali kwa sababu ya rangi walivaa na ndoo hii sababu ya kuandika mada hii mfano Muuzaji wabidhaa Fulani au mtangazaji hutuma ujumbe akitumia rangi Fulani ghafla huamsha hisia za wateja wake hivyo soko la bidha kuongezeka sana na kinyume chake ni sawa.Kama ilivyo kifo na kodi huwezi kuvikwepa na matokeo ya matumizi ya rangi huwezi kuyakwepa daima ;Duniani kuna rangi kuu zifuatazo nyeupe,nyekundu,bluu,njano,green,kutokea hapa rangi nzote nyingine zinatoke hapa kwa mchanyiko wa hizo hapo rangi mfano pink,majivu nakadhalika,mara nyingi inashauriwa kuvaa rangi hizo kuu maana zinatoka ujumbe kamili,kila rangi ina maana kubwa kwenye haya maumbile ya dunia,maumbile ya dunia yanafuata kanuni na yatakupatiakile unakihitaji kulingana na lugha yako.Zifuatazo ni aina za rangi na matumizi yake mahala tofauti na shughuli tofauti,
1.Nyekundu:Inatoa ishara ya hisia kali,amri,nguvu,amri,uchokozi:
Hii rangi hutumika sana sana katika shughuli za kiutawala
katika kutoa amri au kusisitiza jambo Fulani lifanyike upesi na kimakini sana,mfano
bosi ofisini anaweza toa amri kwa wafanyakazi wake ofisini jambo Fulani lenye
tarehe ya makubaliano lifanyike upesi au katika jambo ambalo kama vile watu
hawataki Huku amevalia tai nyekundu.Pia kwa kiongozi wanchi anapoenda toa amri
jambo Fulani lifanyike kwa baraza la mawaziri huvaa tai nyekundu hivyo hivyo
kwa mawaziri kwa walio chini yao .Hii rangi sio nzuri katika majadaliano ya
jambo Fulani ili kufikia muafaka(negotiation) na wewe upo chini ya mtu
uliyemvalia nyekundu mfano mwaka
2009 Barack Obama na raisi wa Urusi
Drimitry Medved walipokuwa pale marekani kufanya majadiliano ya kibiasha kati
ya nchi zao Obama alivaa tai nyekundu
(alikuwa na sauti kubwa maana yake) na raisi
wa Urusi alivaa blue hii ilikuwa mawasiliano tosha tuu na hawakuvaa
kibahati ilikuwa impangiliwa hivyo
.
2. Bluu (Blue):Mawasiliano juu ya hisia zako za
kweli,Uaminifu,upole au utulivu wa ndani wa mtu,wajibu,utii,mantiki,huruma.
Ni rangi
ya ulizi hii ni rangi muhimu sana ya wewe
uonewe huruma na watu wengine,mathalani hutumiwa kwenda kuomba kazi kwa
kampuni
mbalimbali ni vema ukavaa tai ya blue kipindi cha interview,Blue pia
huvaliwa
kipindi cha ujenzi na mafundi ndoo maana overall la kwanza kabisa
lilikuwa la
rangi ya blue ikiwa na maana ya ulizi(protection).Blue pia hutumika
kipindi cha
wewe kusafiri kwenda sehemu mbalimbali unasafiri ,Katika majadiliano ya
biashara
au mengine kama wewe sio mwenye mali au (sauti katika hayo) inashauriwa
kuvaa blue huruma itawajia wale unaofanya nao mazungumzo
na mazunguzmo kwenda vizuru sana kwa uaminifu mkubwa sana .
3.Njano:Umakini(focus)
wa jambo Fulani, nguvu za mtu binafsi hisia,kujiamini kwa mtu yeye mwenye ndani
yake, chanya,kujiamini,ubunifu,urafiki,matumaini.
Hii hutumika kama unataka watu waweke umakini kukusikiliza wewe na
kuelewa kile unachokisema sana sana
kwenye hotuba,mahubiri,semina,mikutano nk ni rangi husika kuvuta umakini kutoka
kwa watu,huchochea spidi za metaboli mwilini,vile vile njano hutumika katika
kusoma,au kuwa makini juu jambo Fulani hivyo kuonyeshea wengine kuwa wewe upo
katika hali ya kutotaka usumbufu wa aina yeyote ile na hivyo kukuacha na umakini wako,mfano ukiwa unasoma
unashauriwa kama hutaki usumbufu kutoka kwa rangi ya njano ni sahihi.
4.Majani(Green):Kusambaa(expand),uwiano,amani,kusonga
mbele.
Rangi muhimu sana inayomaanisha kuzidi kukua na kuimarika
mfano kampuni au jambo Fulani.Green ni rangi ya mimea na mimea imeenea kote ulimwenguni hivyo green
katika maumbile ya dunia inamaana ya kusambaa au kukua na kuimarika mfano pale
kampuni inapotaka kukua kwa kasi na
kusonga mbele kwa kasi utakuta
wafanyakazi wamevalia t-shirt green hapa kuna maana kubwa sana kwa
maumbile ya dunia,Kenya ilipopitisha na kuanza kuyatekeleza maono(vision)2030
iliweka rangi ya green hii ilikuwa na
maana kubwa sana katika maumbile ya dunia kuwa Kenya inazidi kukua na kusonga
mbelembele hii rangi Kenya haikuweka
kibahati ni plan ya wao kuendelea.
5. Nyeupe: Chanya, usafi wa mtu ndani
,halisi,uwazi,urahisi au wepesi,ufanisi.
Hapa ni dalili wa uwepo wa rangi zote hutokana,nyeupe
hutumika katika maeneo ya ibada,sherehe za amani na furaha,nini nyeupe ina
maani kwa maumbile ya dunia?nyeupe inaonyesha usafi wa mtu rohoni,utayari wa
kusaidia watu wengine,amani ya mtu kwa watu,yaani mambo yapo salama,pendelea
kuvaa nyeupe wakati wa ibada za kufunga,meditation,sherehe za kusaidiaa watu
wenye shida,sherehe na matukioyanayo
maanisha amani
Wengi nazani mtajiuliza je nyeusi je?nyeusi ni kutokuwepo kw
rangi yeyote,hivyo nyeusi si rangi,katika maumbile ya dunia huja yaambia jambololote
lile hivyo lolote lile linaweza kukuadhiri wewe kwa sababu haupo kwa rangi
yeyote,
Mchanyiko wa hizo rangi hapo juu ndoo tuna pata rangi
nyingine chungu nzima mfano pink hutumika wakatik machombezo na mpenzi
wako,ukiwa upo ndani pink ni rangi ya mahaba na ni nzuri wapenzi wakiivalia
wakiwa katika stori za mahaba.
Matuki na aina za rangi
- Interview-blue sanasana ukivaa tai ya bluu na shati jeupe.
- Kutoa amri-nyekundu
- Kuhutubia/kufundisha-njano
- Kukua na kuimarika-green
- Kusaidia jamii-nyeupe/bluu
Maarifa ni kitu endelevu,kila siku kuna jambo linaendeleakatika tafiti,maisha ni kanuni nzuri zaidi kuwepo ndani ya hizo kanuni.Ukitaka kuendele mafanikio yapo mikononi mwako amua leo.
0 comments:
Post a Comment